Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtalamu wa UM aitaka Kenya kuwashughulikia wakimbizi wa ndani

Mtalamu wa UM aitaka Kenya kuwashughulikia wakimbizi wa ndani

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa Chaloka Beyani ameishauri serikali ya Kenya kuweka mikakati ya kushughulikia changamoto zinazowakumba wakimbizi wa ndani nchini humo.

Mtaalamu huyo aliyetwikwa jukumu na baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa kutoa ripoti kuhusu hali ya wakimbizi wa ndani amesema kuwa kuna haja ya kushughulikia hali na haki za wakimbizi wa ndani nchini Kenya wakiwemo waliothiriwa na ghasia za mwaka 2008 , wale waliolazimika kuhama kutokana na majanga ya kiasili na waliotimuliwa kutoka kwenye misitu. George Njogopa anaripoti.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)