Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maradhi yasiyo ya kuambukiza ni changamoto Tanzania:Mponda

Maradhi yasiyo ya kuambukiza ni changamoto Tanzania:Mponda

Magonjwa yasiyo ya kuambukiza yaani NCD's kama saratani, kisukari, maradhi ya moyo na matatizo ya kupumua sasa yamekuwa changamoto kubwa kwa mataifa yanayoendelea.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa maradhi hayo ambayo yalikuwa zaidi katika mataifa tajiri sasa yamegeuza mwelekeo na kuzikumba nchi masikini ambazo nyingi haziwezi kumudu kukabiliana na magonjwa hayo.

Miongoni mwa mataifa hayo ni Tanzania ambako waziri wa afya wa nchi hiyo mheshimiwa Haji Mponda amesema imebidi serikali kuweka mikakati kwani kila kati ya watu 10 watatu wanamaradhi hayo.

Akizungumza na Idhaa hii amesema elimu kwa umma ni muhimu hasa ya kupima na kujua nini wanapaswa kufanya kuepuka maradhi hayo. Sikiliza sehemu ya kwanza ya mahojiano hayo kati ya waziri Mponda aliyehudhuria mjadala wa Umoja wa Mataifa kuhusu magonjwa hayo hapa New York na Flora Nducha.

(MAHOJIANO NA WAZIRI HAJI MPONDA)