Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yasambaza misaada kwa walioathirika na mafuriko Pakistan

IOM yasambaza misaada kwa walioathirika na mafuriko Pakistan

Usambazaji wa misaada kwenye maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko mkoani Sindh nchini Pakistan ukiendelea shirika la kimataifa la uhamiaji IOM linasema kuwa serikali ya Pakistan inakadiria kuwa idadi ya walioathirika na mafuriko imefikia watu milioni 8.

IOM inashirikiana na kikosi cha wanajeshi wanamaji nchini Pakistan kusambaza mahema 1000 na bidhaa zingine kwa watu waliokwama vijijini katika eneo la Tando Bago wilayani Badin. Msaada huo ndio wa kwanza kimataifa kufikia vijiji ambavyo bado viemzungukwa na mafuriko tangu mwezo Agosti. Jumbe Omari Jumbe ni afisa wa IOM

(SAUTI YA JUMBE OMARI JUMBE)