Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

China yataka nchi za G 20 kuwa mshirika muhimu kwenye uchumi wa dunia

China yataka nchi za G 20 kuwa mshirika muhimu kwenye uchumi wa dunia

Fungamano na nchi 20 ambazo ziko kwenye alama ya usoni kuchipukia kwenye masuala ya uchumi wa viwanda na maendeleo jumla ya kiuchumi, zinapaswa kuwa na sauti kubwa kwenye masuala ya uchumi wa dunia. Hayo ni kwa mujibu wa waziri wa mashauri ya kigeni wa China Yang Jiechi ambaye ameyasema wakati akizungumza kwenye mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa New York.

Waziri huyo wa kigeni amezitaka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuweka shabaya ya pamoja ili kuyafikia malengo ya kimaendeleo. Amesema pale panapohusika na masuala ya uchumi wa dunia, lazima nchi zinazochipukia kiviwanda yaani G 20, zihusike moja kwa moja na zinapaswa kufanya hivyo kwa kuangalia uzito wao.