Baraza la Usalama lajadili ombi la taifa la Palestina

26 Septemba 2011

Ombi la Palestina kuwa mwanachama kamili wa Umoja wa Mataifa linajadiliwa mchana huu kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Rais wa Palestina Mahmoud Abbas aliwasilisha ombi la kutambulika kama taifa kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon Ijumaa iliyopita. Majadiliano hayo yamefanyika kwa faragha.

Kura tisa zinahitajika zikiwemo za wajumbe wote watano wa kudumu kati ya wajumbe 15 wa Baraza la Usalama ili baraza hilo liweze kupendekeza kujumuishwa kwa Palestina kuwa mwanachama. Na pendekezo hilo litawasilishwa kwa wajumbe 193 wanachama wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Wajumbe wa kudumu wa baraza hilo ni China, Ufaransa, Urusi, Uingereza na Marekani. Marekani tayari imesema itatumia kura ya turufu kuzia ombi hilo. Marekani inaunga mkono taifa la Palestina lakini inasema lazima Palestina ijadiliane na Irsrael kuhusu suala hilo.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter