Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban, Odinga wajadilia hali ya Pembe ya Afrika

Ban, Odinga wajadilia hali ya Pembe ya Afrika

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekuwa na majadiliano na Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga kuhusu hali jumla ilivyo katika eneo la Pemba ya Afrika ikiwemo pia vitendo vya utekaji nyara wa meli katika pwani ya Somalia. Katika majadiliano hayo viongozi hao wawili pia walibalishana mawazo kuhusu hali ya mkwamo wa chakula inayoliandama eneo hilo.

Wakikutana kandoni mwa mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa unaendelea mjini New York, Ban na Odinga walitumia fursa hiyo kujadilia mwenendo wa utelezwaji wa katiba mpya ya Kenya na maandalizi ya uchaguzi mkuu wa mwakani. Katika upande mwingine, Ban alikutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Montenegro na kujadilia masuala mbalimbali ikiwemo juu ya utekelezaji wa mpango wa utoaji huduma wa pamoja unaoendeshwa sasa na Umoja wa Mataifa.