Shambulizi la mabomu nchini Iraq lalaaniwa:UM

26 Septemba 2011

Kaimu mkuu wa huduma za Umoja wa Mataifa nchini Iraq amelaani vikali shambulizi la kigaidi la mwishoni mwa juma lililolenga majengo ya serikali kwenye mji wa Karbala na kuwaua zaidi ya watu 10 na kuwajeruhi wengine kadha. Jerzy Skuratowicz pia ametuma rambi rambi zake kwa familia za wahanga wa shambulizi hilo na kuwatakia nafuu ya haraka waliopata majeraha.

Ripoti za vyombo vya habari zinasema kuwa mabomu yalilipuliwa kwenye mji wa Karbala huku matatu kati yao yakilipuka wakati poilisi na wafanyikazi wa mambo ya dharura walipofika baada ya mlipuko wa kwanza.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud