Hali ya kibinadamu Yemen inazidi kuzorota:UM

Hali ya kibinadamu Yemen inazidi kuzorota:UM

Hali ya kichumi na kibinadamu inaendelea kuzorota nchini Yemen limesema Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Wajumbe 15 wa baraza hilo wametoa taarifa usiku wa Jumamosi wakitaka utulivu urejeshwe katika taifa hilo la Ghuba linalokabiliwa na machafuko hivi sasa.

Baraza hilo limesema kumekuwa na hali ya hatihati, mvutano na kuendelea kwa machafuko kufuatia kurejea nyumbani siku ya Ijumaa Rais Ali Abdullah Saleh ambaye amekuwa nje ya nchi kwa miezi mitatu sasa.