Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM na Lonely Planet wazindua ushirikiano

UM na Lonely Planet wazindua ushirikiano

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA na mchapishaji mkubwa na masuala ya usafiri Lonely Planet leo wametazanga kuzindua ushirikiano wa kusaidia kutoa taarifa muhimu kwa wanaochukua hatua za misaada ya dharura.

OCHA inakusanya na kuratibu juhudi za misaada ya dharura duniani na kupeleka watu wa kwanza wa kimataifa kutoa misaada knakohitajika.

OCHA imesema kwa shirikiano huo sasa wafanyakazi wa mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa, serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali yanayotoa misaada ya kibinadamu ambayo hufika katika tukio katika muda wa saa 24 sasa yataweza kutumia taarifa za lonely Planet kufahamu zaidi  kuhusu eneo hilo, mazingira, historia, miundombinu na utamaduni ambazo ni taarifa muhimu kabla ya kusafiri kwenda kutoa msaada.

Ushirikiano huo umezinduliwa kwenda sambamba na siku ya kimataifa ya utalii ambayo huadhimishwa kila mwaka Septemba 27.