Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO imetoa wito wa kuboresha hali ya hewa mjini kwa ajili ya afya

WHO imetoa wito wa kuboresha hali ya hewa mjini kwa ajili ya afya

Katika miji mingi duniani uchafuzi wa hali ya hewa imefikia kiwango cha kutishia maisha ya watu zimesema takwimu zilizokusanywa na shirika la afya duniani WHO. Takwimu hizo zilizotolewa leo zinajumuisha zile zilizokusanywa kutoka karibu miji 1100 katika nchi 91, ikiwemo miji mikuu na miji midogo yenye wakazi zaidi ya 100,000.

WHO inakadiria kwamba watu zaidi ya milioni 2 wanakufa kila mwaka kutokana na kuvuta hewa yenye chembechembe za uchafu ndani na nje. Dr Maria Neira ni mkurugenzi wa afya ya jamii na mazingira wa WHO.

(SAUTI YA DR MARIA NEIRA)