Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mabadiliko katika serikali yanatoa fursa kiuchumi kwa wanawake:Bank ya dunia/IFC

Mabadiliko katika serikali yanatoa fursa kiuchumi kwa wanawake:Bank ya dunia/IFC

Ripoti mpya iliyotolewa leo na Bank ya dunia na IFC imebaini kwamba wanawake bado wanakabiliwa na vikwazo vya sera na kisheria katika kushiriki kikamilifu kwenye masuala ya uchumi. Ripoti hiyo iitwayo “wanawake, biashara na sheria 2012, kuondoa vikwazo katika kujumuisha wote kwenye uchumi” imebaini kwamba wakati mataifa 36 yamepunguza tofauti za kisheria baina ya wanawake na waname, nchi 103 kati ya 141 zilizofanyiwa utafiti bado zina vikwazo vya tofauti za kisheria kwa misingi ya jinsia .

Ripoti hiyo pia imeainisha mabadiliko 41 ya sera na sheria yaliyopitishwa kati ya Juni 2009 na Machi 2011 ambayo yataweza kuinua nafasi za wanawake katika uchumi. Kimataifa wanawake wanawasilisha asilimi 49.6 ya watu wote duniani lakini ni asilimi 40.8 tuu ya wanawake ndio walio katika sekta zisizo rasmi, hii ni kutokana na tofauti zinazosababishwa na masuala ya sheria kati ya wanawake na wanaume.

Hata hivyo ripoti imesema kuna baadhi ya sehemu hatua imeenza kupiga kondoa tofauti hizo ikiwemo Amerika ya Kusini, Caribbean, Ulaya na Asia ya Kati.