Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali ya kibinadamu Libya imeanza kuimarika:UM

Hali ya kibinadamu Libya imeanza kuimarika:UM

Hali ya kibindamu Libya imeanza kuimarika isipokuwa tu kwenye maeneo ambayo mapigano bado yanaendelea umesema Umoja wa mataifa. Mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Matiafa Libya Panos Moumtzis amesema kumekuwa na hatua kubwa ya kimarika kwa hali kwenye ugawaji wa chakula, maji na kupata huduma za afya.

Kwa uwezo wa baraza la kitaifa la mpito linaloongoza Libya kwa sasa kuweza kukabiliana na mahitaji ya kibinadamu kunaongeza matumaini kwa Umoja wa Mataifa ya kumaliza hatua ya operesheni zake za mgogoro wa Libya ifikapo mwezi Novemba mwaka huu. Hata hivyo amesema raia wanakabiliwa na hatari kubwa kutokana na mabomu ya ardhini ambayo hayajateguliwa na silaha zingine zilizosalizwa na vita.

Bwana Moumtzis amesema kuwa timu maalumu ya Umoja wa Mataifa inayohusika na mabomu ya ardhini imepelekwa Libya kuanza kutegua mabomu hayo.

(SAUTI YA PANOZ MOMTZIS)

Bwana Moumtzis amesema serikali ya Marekani imekubali kuachilia dola bilioni 1.5 za Libya inazozizuilia ili kusaidia mipango ya mahitaji ya kibinadamu ikiwa ni pamoja na kununua mafuta na kulipa mishahara.