Uchaguzi wa Zimbabwe lazima uwe huru na wa amani:Ban

24 Septemba 2011

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesisitiza kuwa uchaguzi wa bunge unaotarajiwa kufanyika nchini Zimbabwe lazima uwe wa huru na wa haki. Katika mkutano na Morgan Tsvangirai, Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Ban ameeleza haja ya uchaguzi wa haki na wa kuaminika usiokuwa na vita wala vitisho.

Ban na Tsvangirai pia wamejadili utekelezaji wa mkataba wa kisiasa (GPA), mkataba uliotiwa saini mwaka 2009 na kusababishwa kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa katika taifa hilo la kusini mwa Afrika na kumaliza mgogoro wa kisiasa ambao ulifuatiwa uchaguzi uliopita. Katika mkutano wao viongozi hao wawili wamejalili kwa ujumla hali ya kijamii na kiuchumi nchini Zimbabwe.

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter