Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kukabidhiana madaraka kwa amani Zambia baada ya uchaguzi ni mfano wa kuigwa:Ban

Kukabidhiana madaraka kwa amani Zambia baada ya uchaguzi ni mfano wa kuigwa:Ban

Zambia imeweka mfano wa kuigwa kwa bara zima la Afrika na dunia kwa jumla wa jinsi gani madaraka yanaweza kukabidhiwa kwa njia ya amani baada ya uchaguzi. Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon akiwapongeza watu wa Zambia kwa kukamilisha uchaguzi mkuu wa Rais.

Mpinzani wa muda mrefuu Michael sata ndiyo Rais mpya baada ya kumshinda kwa kura chache mpinzani wake Rupiah Banda zimesema duru za habari.

Katika taarifa yake Ban amewapongeza Wazambia kwa kupiga kura katika mazingira ya amani na mpangilio mzuri, na ameipongeza pia tume ya uchaguzi ya nchi hiyo kwa jukumu kubwa lililokuwa nalo kuhakikisha uchaguzi huo ni wa huru, wazi na wa haki.

Ban amempongeza Rais mpya bwana Sata kwa ushindi na bwana Banda kwa kukubali kushindwa. Na amesema amefurahishwa kwamba Zambia imelionyesha baraza la Afrika na dunia kwamba mabadiliko yanaweza kuletwa kwa njia ya amani endapo demokrasia itapewa nafasi.