Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Viongozi wa dunia wajadili mgogoro wa kibinadamu wa Pembe ya Afrika

Viongozi wa dunia wajadili mgogoro wa kibinadamu wa Pembe ya Afrika

Viongozi wa dunia na wawakilishi wa mashirika yanayohusika na misaada ya kibinadamu wanaokutana kwenye Umoja wa Mataifa kuhudhuria mjadala wa Baraza Kuu leo Jumamosi wamejadili mtafaruku wa kibinadamu unaoikabili Pembe ya Afrika.

Viongozi hao wamesisitiza haja ya kuongeza juhudi kukabiliana na janga hilo la kibinadamu lililosababishwa na njaa na vita katika ukanda huo. Pia wametathimini jinsi gani jumuiya ya kimataifa imekabiliana na mahitaji ya dharura ya kibinadamu yanayohitajika Djibouti, Ethiopia, Kenya na Somalia nchi ambazo ni waathirika wakubwa. Mkutano huo ambao pia umechangisha fedha umesema dola takribani milioni 700 zinahitajika kuendelea kusaidia katika Pembe ya Afrika kama anavyofafana Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon akizungumza kwenye mkutano huo.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

Naye waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga anayeiwakilisha nchi yake katika mkutano huo, amesema taifa lake ambalo limekuwa likibeba mzigo wa wakimbizi kutoka Somalia tangu mwaka 1991 sasa linalemewa, na jumuiya ya kimataifa inahitaji kunyoosha mkono zaidi kusaidia. Pia amesema suluhisho la ndani ya Somalia ni muhimu zaidi

(SAUTI YA RAILA ODINGA)