Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sudan Kusini haitoingilia mgogoro wa Kordofan:Kiir

Sudan Kusini haitoingilia mgogoro wa Kordofan:Kiir

 

Rais mpya wa Sudan Kusini Salva Kiir amesema nchi yake haitoingilia mgogoro unaoendelea kati ya Kordofan Kusini na Sudan. Sudan Kusini imepata huru wake kutoka Kaskazini mwezi Julai mwaka huu na imekuwa ikijaribu kupatanisha jamii zilizogawanyika.

Rais Salva Kiir amesema amekutana na Rais wa Marekani Barrack Obama kujadili migogoro ndani ya nchi yake na ndani ya Sudan. Pia Rais Kiir ameiomba jumiya ya kimataifa kusaidia katika kuijenga upya Sudan Kusini na kuleta maridhiano.

Amesema taifa hilo ambalo bado changa likiwa na umri wa miezi miwili na 14 hii leo Septemba 23 linahitaji kila aina ya msaada kuweza kusimama peke yake.