Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi 20 zajitolea kulinda maji yao:UM

Nchi 20 zajitolea kulinda maji yao:UM

Nchi 20 na mashirika 4 waliohudhuria mkutano wa mawaziri mjini Astana wamekubaliana na hatua 75 za kuimarisha maji yao. Hatua hizo zinahusika na maji na sehemu za maji, maji na afya na kupata maji na usafi miongoni mwa makubaliono mengine.

Makubaliano hayo yanaafikiwa baada ya changamoto zilizotambulika kwenye ukaguzi wa mito na maji ya chini ya ardhi yanayopita zaidi ya nchi nchi moja. Kati ya nchi zenye makubalino Finland imejitolea kuchunguza matumizi ya maji na kutoa onyo ya majanga ya kiasili.