Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM na wanajeshi wa Pakistan watoa misaada kwa waathiriwa wa mafuriko

IOM na wanajeshi wa Pakistan watoa misaada kwa waathiriwa wa mafuriko

Kundi kutoka shirika la kimataifa la uhamiaji IOM linashirikiana na wanajeshi wanamaji nchini Pakistan kuwapelekea misaada ya chakula na bidhaa zingine waathiriwa wa mafuriko katika wilaya ya Badin kwenye mkoa wa Sindh.

Misaada hiyo ikiwemo blanketi na vyombo vya jikoni ndiyo ya kwanza kimatiafa kuwafikia waathiriwa wa mafuriko kwenye vijiji vya Judho ambavyo vimezungukwa na mafuriko tangu mwezi Agosti. Inakadiriwa kuwa watu 1.7 wameathiwa na mafuriko wengi wakiwa ni watu maskini na familia zao.  Jumbe Omari Jumbe ni afisa wa IOM.

(SAUTI YA JUMBE OMARI JUMBE)