Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Serikali ya Burundi imetakiwa kukumbatia mazungumzo ili kusitisha ghasia:UM

Serikali ya Burundi imetakiwa kukumbatia mazungumzo ili kusitisha ghasia:UM

Serikali ya Burundi imetakiwa kufanya mashauriano na upande wa upinzani ili kuzuia kile ambacho kinaonekana kama kusambaa kwa ghasia na mauaji. Ofisi ya kutetea haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imesema kuwa mauaji yaliyofanyika juma hili ya watu 38 katika eneo la Gitumba magharibi mwa mji mkuu Bujumbura ni ishara ya kuongezeka kwa ghasia nchini Burundi.

Mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay anasema ghasia hizo ni za kutia wasi wasi kwa kuwa zinaonekana kuwalenga wafuasi wa chama cha upinzani cha National Liberation Front. Ravina Shamdasani ni kutoka ofisi ya haki za binadamu ya UM

(SAUTI YA RAVINA SHAMSADAN)