Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mawaziri wa mambo ya nje wa G77 na Uchina wajadili matatizo yanayoikabili dunia hivi sasa

Mawaziri wa mambo ya nje wa G77 na Uchina wajadili matatizo yanayoikabili dunia hivi sasa

Mawaziri wa mambo ya nje wa kundi la G77 na Uchina wamekutana leo kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili dunia hivi sasa. Miongoni mwa changamoto hizo ni mabadiliko ya hali ya hewa, matatizo ya uchumi, bei za vyakula na hali ya Pembe ya Afrika.

Akizungumza katika mkutano huo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema wiki hii ambapo viongozi wa dunia wako New York kwenye mjadala wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa changamoto hizo zimekuwa msitari wa mbele na hasa suala la maendeleo ambalo amesema lina nadafi kubwa katika G77.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

Ameongeza kuwa vijana ambao ni muhimu kwa mustakhbali wa dunia wanakosa fursa wanaostahili na wengi wao wanachanganyikiwa na shinikizo la maisha, hali ambayo inaweza kuchochea machafuko. Hata hivyo amesema endapo kutakwa na muongozo na msaada, hali hiyo inaweza kubadilishwa na kuleta mabadiliko mazuri.