Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mexico yaiomba UM kusaidia kukabili madawa ya kulevya

Mexico yaiomba UM kusaidia kukabili madawa ya kulevya

Mexico imewasilisha ombi kwa Umoja wa Mataifa ikita isaidiwe kukabiliana na wimbi kubwa la silaha pamoja na matumizi ya madawa ya kulevya, ambayo yote kwa pamoja yamesababisha maelfu ya watu kuuawa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita. Ripoti kutoka nchini humo zinasema kuwa maelfu ya watu waliowawa kikatili katika kile kinachoelezwa vita vya madawa ya kulevya.

Taifa hilo hivi sasa linaomba Umoja wa Mataifa kuweka nguvu yake ili kudhibiti uzalishaji na usafirishaji wa madawa ya kulevya ambayo yapo kwa kiwango kikubwa. Rais wa Mexico Felipe Calderón ameuambia mkutano wa baraza kuu mjini New York kuwa mamia ya watu wanaendelea kupoteza maisha kutokana na biashara chafu ya madawa ya kulevya ambayo wahusika wake hujipatia silaha na dhana nyingine hatari.