Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban amtaka Waziri Mkuu wa Israel kuweka utashi wa busara mbele wakati wa kujadilia ombi la Palestina la kuwa mwanachama wa UM

Ban amtaka Waziri Mkuu wa Israel kuweka utashi wa busara mbele wakati wa kujadilia ombi la Palestina la kuwa mwanachama wa UM

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amemtaka Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyau kuzingatia busara na utashi wa kisiasa wakati wa kujadilia hali ya Palestina ambayo imepanga kuwasilisha ombi lake la kuwa mwanachama wa Umoja huo wa Mataifa.

Wakikutana kwa faragha kandoni mwa mkutano wa 66 wa Baraza Kuu unaoendelea mjini New York, Ban alimweleza Waziri huyo Mkuu wa Israel kuwa Umoja wa Mataifa unapenda kuona pande zote mbili zinaendelea kuishi kwa amani na maelewano makubwa. Amesema kuwa mazungumzo ya mezani ndiyo njia bora itayosaidia kukwamua mkwamo unaendelea kwenye eneo hilo na siyo vinginevyo.

Kiongozi wa Mamlaka ya Palestina anapanga kuwasilisha ombi maalumu kwenye mkutano huu akitaka taifa hilo lipewe uawanachama wa Umoja wa Mataifa.