Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban awataka wanasiasa Madagascar kutekeleza kwa vitendo makubaliano ya amani

Ban awataka wanasiasa Madagascar kutekeleza kwa vitendo makubaliano ya amani

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekaribisha mpango wenye shabaya ya kumaliza mkwamo wa kisiasa nchini Madagascar lakini amezitolea mwito pande zote kuweka shabaha ya pamoja ili uchaguzi ulio huru na haki unafanyika. Baada ya kujiburuta kwa muda mrefu hatimaye vyama vya kisiasa nchini humo vimesaini makubaliano ya amani, chini ya upatanishi wa Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SADC.

Mpango huo unaojulikana kama 'road map', unafungua ukurasa wa kurejea nyumbani bila masharti yoyote kwa rais wa zamani wa nchini Marc Ravalomanana ambaye yuko uhamishoni. Ama makubaliano hayo yanaruhusu kuanzishwa kwa taasisi huru za kipindi cha mpito kuelekea kwenye uchaguzi mkuu hapo baadaye.

Akijadilia hatua hizo, Ban pamoja na kupongeza juu ya hatua hiyo iliyopigwa lakini amesisitiza kwa pande zote kutouangusha mpango huo akitaka kila upande utekeleze jukumu lake.