Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tanzania imechangia pakubwa katika suluhu ya migogoro na kutafuta amani:Kikwete

Tanzania imechangia pakubwa katika suluhu ya migogoro na kutafuta amani:Kikwete

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete amesema serikali yake imechangia pakubwa katika jitihada za kuleta amani Afrika, ikiwa ni pamoja na kutatua mgogoro na kuchangia vikosi vya kulinda amani. Akihutubia mjadala wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa hii leo, pia amesema Watanzania wanaamini watu wote wako sawa, wanastahili uhuru na amani kama walivyo wengine. Kuhusu suala la Palestina kuwa na taifa huru Rais Kikwete amesema Tanzania inaunga mkono suala la kuwa na taifa huru la Palestina litakaloishi kwa amani na usalama na jirani zao Israel.

(SAUTI YA RAIS JAKAYA KIKWETE)

Rais Kikwete pia amesema kwa miaka 50 Tanzania imekuwa mwanachama wa Umoja wa Mataifa na itaendelea kutimiza wajibu wake katika Nyanja mbalimbali ikiwemo kuchagiza maendeleo, ikiwa ni pamoja na kuwawezesha wanawake, masuala ya afya na kutimiza malengo ya maendeleo ya milenia, amezitaka nchi zilizoendelea kutimiza ahadi zake za kusaidia nchi masikini ili nazo zijikwamue. Masuuala mengine aliyojadili ni pamoja na tatizo la njaa Pembe ya Afrika, vita Somalia, uharamia na ugaidi wa kimataifa.