Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza Kuu la UM lajadili usalama wa nyuklia

Baraza Kuu la UM lajadili usalama wa nyuklia

Mjadala unaoendelea kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, usalama wa nyuklia umepewa kipaumbele. Akizungumza kwenye mjadala huo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon akitolea mfano wa ajali ya kinu cha nyuklia cha Fukushima Daichi iliyosababishwa na tetemeko la ardhi na tsunami Ban amesema kuwa ni lazima kwanza kuhakikisha kuwepo imani kutoka kwa watu.

Ban amesema kuwa wenyeji wa eneo hilo wanaishi kwa hofu ya athari zinazoweza kutokana na mionzi kutoka kwa kinu. Ban amesema kuwa kutimiza malengo haya kunahitaji kuwepo uwazi katika masuala yote ya nguvu za nyuklia. Lakini pia ametaja masuala mengine manne muhimu.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)