Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ubaguzi wa rangi na kutovumiliana kunaendelea

Ubaguzi wa rangi na kutovumiliana kunaendelea

Miaka kumi iliyopita Umoja wa Mataifa ulipitisha azimio la Durban na mpango wa kuchukua hatua dhidi ya ubaguzi wa rangi, ambapo jumuiya ya Kimataifa ilitanabaisha kwamba hakuna nchi ambayo itasema iko huru bila ubaguzi na kutovumiliana. Leo ni miaka kumi na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa unaadhimisha kwa kutathimini hatua zilizopigwa na nini kiendelee kufanyika.

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon amesema suala hili bado ni tatizo ingawa hatua zimepigwa kukabiliana na matatizo ya ubaguzi, mauaji ya wageni na kutovumiliana. Amesema sheria zimeanza kushika mkondo, mipango ya kuchagiza utengamano na watu wamejiandaa vyema sasa kuchukua hatua na kulinda watu dhidi ya mauaji ya kimbari, ubaguzi wa rangi, mauaji ya kikabila na mifumo ya kisasa ya utumwa. Amesema ubaguzi dhidi ya Waafrika, watu wenye asili ya Afrika, Waasia, watu wa asili, wahamiaji, wakimbizi, makundi ya wachache, waromania na wengine lazima ukomeshwe. Na kuongeza kuwa

(SAUTI YA BAN KI-MOON)