Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mikataba zaidi yatiwa sahihi kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa

Mikataba zaidi yatiwa sahihi kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa

Mikataba kumi kuhusu haki za binadamu imetiwa sahihi wakati wa kung’oa nanga wa mkutano wa kila mwaka wa Umoja wa Mataifa ulio na lengo la kuunga mkono mikataba duniani. Taifa la Palau lilikuwa mshiriki aliyetia sahihi karibu mikataba yote ikiwemo mikataba ya kumaliza ubaguzi wa kila aina, ubaguzi dhidi ya wanawake vikiwemo vitendo vya mateso na vingine vinavyokiuka haki za binadamu.

Palau pia ilitia sahihi mkataba wa kimataifa wa kulinda haki za wahamiaji na watu wa familia zao ukiwemo mkataba wa watu walio na ulemavu na kuzuia kutoweka kwa watu.