Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM walaani vikali mauaji ya raia wa zamani wa Afghanistan

UM walaani vikali mauaji ya raia wa zamani wa Afghanistan

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameelezea namna alivyoshtushwa na kupigwa na butwaa kufuatia taarifa za kuuawa kwa rais wa zamani wa Afghanistan Burhanuddin Rabbani, ambaye alisimama mstari wa mbele katika mazunguzo ya usakaji amani wa nchi yake.

Duru za habari zinasema kuwa, kiongozi huyo wa zamani ambaye alikuwa mwenyekiti wa jukwaa la usuluhisho wa migogoro, aliuawa nyumbani kwake Kabul wakati alipokuwa akikutana na wafuasi wa kundi la Taliban kwa ajili ya kujadilia njia za uletaji amani. Mtu aliyekuwa amevisha bomu mwilini mwake, alimsogelea kiongozi huyo na kisha kujilipua. Watu wengine kadhaa walijeruhiwa.

Ban amesema kuwa tukio hilo ni la kusikitisha na limewalenga watu waliojitolea kwa ajili ya kuleta amani.