Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Serena Williams ateuliwa kama balozi mwema wa UNICEF

Serena Williams ateuliwa kama balozi mwema wa UNICEF

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto ( UNICEF ) leo limemteua bingwa wa mchezo wa tennis Bi Serena Williams kama balozi mwema wa kimataifa. Bi. Williams ni mmoja wa wachezaji wa tennis wenye mafanikio ya muda mrefu katika mchezo huu. Mchezaji huyo anayejulikana kwa uwezo wake kuwa mshindi katika mchezo huu, pia anajulikana kwa mchango wake nje ya mchezo.

Mkurugenzi mkuu wa shirika la UNICEF Bw. Anthony Lake amesema kuwa Bi. Williams sio tu bingwa wa tennis lakini ni bingwa kwa watoto, hasa kwa utetezi wa elimu bora kwa watoto. Ameongeza kuwa anafuraha kubwa kwa Bi. Serena kujiunga kama balozi mwema wa Shirika la UNICEF na anatarajia kufanya kazi na Bi. Williams.

Kama balozi mwema wa UNICEF, Bi. Williams atatumia umaarufu na maslahi binfasi kusaidia utetezi wa haki ya elimu kwa watoto ambao ni ujumbe wa shirika hilo, kwa kupitia mpango wa shule Afrika and Asia.