UM kusimama upande wa watu wa Libya:Al-Nasser

20 Septemba 2011

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Nassir Abdulaziz Al-Nasser amesema kuwa Umoja wa Mataifa unawaunga mkono wananchi wa Libya wanapojitolea kupigania taifa bora la siku za baadaye. Viongozi wa mataifa mbali mbali na mawaziri wanajadiliana kuhusu hali ilivyo nchini Libya na njia zinazoweza kutumika kulisaidia taifa hilo kusonga mbele na kuzuia umwagikaji zaidi wa damu.

Nasser amesema kuwa Umoja wa Mataifa umechukua msimamo tangu kuanza kwa ghasia nchini Libya. Lakini hata hivyo nyingi ya nchi za Afrika zina maoni tofauti kuhusu vile mzozo nchini Libya umeshughulikiwa. Moses Wetangula ni waziri wa mambo ya kigeni nchini Kenya na anahudhuria mkutano huo kuhusu Libya.

(SAUTI YA MOSES WETANGULA)

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter