Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kazakhstan yatakiwa kuwekeza kwenye elimu ya wote

Kazakhstan yatakiwa kuwekeza kwenye elimu ya wote

Mtaalamu wa Umoja wa Mataifa juu ya masuala ya elimu Kishore Singh, ameitolea mwito serikali ya Kazakhstan kuongeza ufadhili kwenye sekta ya elimu ili kuimarishwa ustawi wa kidemokrasia unaoanza kuchipua upya nchini humo. Mtaalamu huyo ameitaka serikali hiyo kuweka shabaha ya kufadhilia miradi ya utoaji elimu mbadala itayojumuisha makundi yote ili hatimaye kufikia shabaha ya ukamilivu wa kidemokrasia.

Ametaka kuongeza kuwa vipaumbele vya uwekezaji kwenye maeneo ya elimu na kusisitiza kuwa kwa wakati huu taifa hilo limeimarisha misingi yake ya ukuzaji uchumi ni vyema kufanya hivyo