Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza Kuu la UM la ahidi kupambana na NCD’s

Baraza Kuu la UM la ahidi kupambana na NCD’s

Shirika la Afya duniani (WHO) leo limekaribisha kupitishwa azimio na Umoja Mataifa kupambana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza, ikiwa ni pamoja na magonjwa ya kisukari, moyo, pumu na saratani ambayo kwa ujumla yanaua watu millioni 36 kwa mwaka.

Hii ni mara ya kwanza kwa viongozi wa kimataifa kufikia makubaliano katika baraza kuu la Umoja Mataifa kufikiana kuchukua hatua kupiga vita magonjwa hayo.

Serika zimekubali kufikia haja ya lengo la kimataifa kufuatilia athari za magonjwa hayo na vyanzo vyake kama matumizi ya tumbaku, vyakula vibaya, ukosefu wa mazoezi na madhara ya matumizi ya pombe. Baraza kuu la Umoja mataifa imewaomba shirika la afya duniani (WHO) kuandaa mfumo wa kimataifa utakao tumika katika ufuatiliaji kuendeleza mapambano ya magonjwa hayo kabla ya mwaka 2012. Pia, imetoa mapendekezo kwa ajili ya kuweka lengo ya kimataifa la namna ya kupunguza idadi ya watu wanao athirika na magonjwa hayo.

Viongozi wa kimataifa wameonyesha nia kwa jitihada kubwa ya kuzuia na kutibu magonjwa yasiyo ambukiza kwa kuboresha huduma za afya na kupatikana kwa madawa bora kwa wananchi. Mafanikio yanategemea ushirika wa baina ya sekta zisizo za afya kama mfumo wa fedha, kilimo, usafiri, na maendeleo ya mijini na biashara. Serikali italeta sera zitakazo saidia kupunguza NCD’s katika mipango ya afya kitaifa.

Azimio hii inaonyesha kuwa viongozi wa kimataifa wanaelewa madhara makubwa ya NCDs’ duniani na wana nia ya kuyapunguza. Hatua ya pili sasa ni utekelezaji wa ajenda za kitaifa.