Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mamia ya mahabusu watoweka Libya

Mamia ya mahabusu watoweka Libya

Mamia ya mahabusu waliokamatwa kwa nguvu na majeshi ya kiongozi wa zamani wa Libya Kanali Mammar Gaddafi wamearifiwa kutoweka. Mapigano yanaendelea nchini humo wakati baraza la taifa la mpito likijitahidi kuongeza udhibiti katika maeneo ambayo wafuasi wa Gaddafi wanaleta upinzani.

Jumatatu jaji Philippe Kirsch mjumbe wa kamati ya kimataifa ya uchunguzi kuhusu Libya ametoa taarifa kwenye baraza la haki za binadamuu la Umoja wa Mataifa mjini Geneva kuhusu madai yote ya ukiukwaji wa haki za binadamu yanayodaiwa kufanywa na majeshi yanayomuunga mkono Gaddafi.

Amesema inadaiwa kwamba majeshi hayo yalikamata na kuwashikilia mamia ya Walibya kwenye vizuizi vya barabarani na mjini Tripoli na maeneo mengine. Na waliko wengi wa watu hao hakujulikani. Imeripotiwa pia kwamba mahabusu 19 wamekufa kwa kukosa hewa mwezi Juni mwaka huu.