Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashariki ya kati na uchumi wa kimataifa vyajadiliwa na viongozi wa dunia

Mashariki ya kati na uchumi wa kimataifa vyajadiliwa na viongozi wa dunia

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amejadili mchakato wa amani ya Mashariki ya Kati na hali ya uchumi wa dunia na viongozi wa nchi mbalimbali waliokusanyika New York kwa ajili ya mkutano wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa.

Katika mkutano wake na Sheikh Naser Al-Mohammad Al-Ahmad Al-Sabah, Ban na waziri mkuu wa Kuwait wamethamini maendeleo yaliyopigwa katika kanda hiyo ikiwemo mchakato wa amani, matukio yanayoendelea Syria na uhusiano baina ya Kuwait na Iraq. George Njogopa anaripoti.

(RIPOTO YA GEORGE NJOGOPA)