Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Azimio la UM la kuimarisha usalama wa waandishi wa habari lapitishwa

Azimio la UM la kuimarisha usalama wa waandishi wa habari lapitishwa

Washiriki kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa uliondaliwa mjini Paris wamekubaliana kwa pamoja mpango wa Umoja wa Mataifa wa kuimarisha usalama wa waandishi wa habari na kuhakikisha kuwa ukatili dhidi ya waandishi wa habari unashughulikiwa kisheria. Kulingana na shirika la elimu, Sayansi, na uatamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO ni kuwa zaidi ya waandishi 500 wa habari wameuawa kwa muda wa muongo mmoja uliopita.

UNESCO pia inasema kuwa waandishi zaidi wa habari wamedhulumiwa , wakatekwa, wakakamatwa na kuzuiliwa kinyume na sheria. Pia kampeni za kuhamasisha zinatarajiwa kuendeshwa na nchi wanachama, mashirika ya kijamii na yasiyokuwa ya kiserikali kuhusu uhuru wa kusema na usalama wa waandishi habari.