Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Yemen yalaumiwa kwa ghasia za kuwasaka waandamanaji

Yemen yalaumiwa kwa ghasia za kuwasaka waandamanaji

Serikali ya Yemen imelaumiwa na wajumbe wa baraza la haki za binadamu kwa ghasia za kuwasaka na kuwakandamiza waandamanaji wanaoipinga serikali. Wakijadili ripoti ya ofisi za haki za binadamu za Umoja wa mataifa kuhusu hali ya Yemen wajumbe wa baraza hilo wametoa wito wa kusita mara moja mashambulizi dhidi ya raia, vitendo vya kuwakamata, kuwaweka kizizini, kuwatesa na mifumo yote ya unyanyasaji dhidi ya watu hao wanaoandamana kwa amani.

Naibu Kamishina mkuu wa haki za binadamu Kyung-wha Kang amesema jumuiya ya kimataifa isitofautiane kwa mgogoro unaowakabili watu wa Yemen. Amelitaka baraza kusaidia kuanzishwa kwa uchunguzi huru wa kimataifa ili kufuatilia ukiukaji wa haki za binadamu nchini Yemen kwa lengo la kuhakikisha wahusika wa ukiukwaji huo wanawajibishwa.

(SAUTI YA KYUNG-WHA KANG)