Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM waomba dola millioni 357 kukabiliana na mafuriko Pakistan

UM waomba dola millioni 357 kukabiliana na mafuriko Pakistan

Jimbo la Sindh nchini Pakistani limelemewa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua za monsoon, Umoja wa Mataifa umezindua ombi la msaada wa dola milioni 357 ili kutoa msaada wa kuokoa maisha kwa mamilioni ya waathirika wa mafuriko nchini humo. Mpango huo wa dharura wa Umoja wa Mataifa una lengo la kusaidia kutoa chakula, maji, vifaa vya usafi, msaada wa afya na makazi ya dharura kwa familia zilizoathirika zaidi kwa kipindi cha miezi sita.

Inakadiriwa kwamba watu milioni 5.4 wameathirika na mafuriko kwenye majimbo ya Sindh na Baluchistan. Karibu nyumba milioni moja zimeharibiwa na ekari milioni 4.2 za kilimo zimefurika. Na kufikia sasa watu takribani milioni moja wameachwa bila makazi na wanaishi katika mahema. Elizabeth Byrs ni msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA.

(SAUTI YA ELIZABETH BYRS)