Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wawakaribisha wanachama wake kuridhia mkataba wa kimataifa

UM wawakaribisha wanachama wake kuridhia mkataba wa kimataifa

Wakikutana kwenye mkutano wa kila mwaka wa Umoja wa Mataifa Mjini New York, wakuu wa nchi wanachama wa Umoja huo wamepewa shime kuridhia mikataba mbalimbali ya kimataifa ikiwemo ile inayohusu haki za binadamu.

Wakuu  hao wa nchi wameomba kuweka zingatio juu ya mikataba ya kimataifa ambayo inahimiza mashirikiano ya dhati katika maeneo ya haki za binadamu, kupambana na ugaidi, usalimishaji wa silaha na ulinzi wa mazingira.

Mkutano wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa unatazamiwa kuanza wiki hii ukiwaleta pamoja wakuu wa nchi wanachama ambao wanatazamia kujadilia masuala mbalimbali.