Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Matatizo ya uchumi sio sababu ya kutosaidia maskini:UM

Matatizo ya uchumi sio sababu ya kutosaidia maskini:UM

Matatizo ya kimataifa ya uchumi hayawezi kuwa sababu ya nchi tajiri kutozisaidia nchi maskini kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon.

Leo Ijumaa Ban amezindua ripoti ya kikosi cha utendaji kilichoundwa mwaka 2007 kutathimini maendeleo ya kufadhili malengo ya maendeleo ya milenia ya kupambana na umaskini yaani MDG’s.

Ban amesema ingawa mwaka jana wahisani wametoa dola bilioni 129 katika msaada wa maendeleo bado kuna pengo kubwa kutokana na ahadi zilizotolewa.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

Katibu Mkuu amesema wahisani wengi wanapanga kudhibiti kiwango cha msaada wanaotoa katika miaka mitatu ijayo, wakati ambao watu na nchi maskini zinauhitaji zaidi.