Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Somalia imeenza kupiga hatua kuelekea amani ya kudumu:Mahiga

Somalia imeenza kupiga hatua kuelekea amani ya kudumu:Mahiga

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Balozi Augustine Mahiga amesema wahenga hawakukosea kunena atafutaye hachoki akichoka keshapata, akiuelekeza msemo huo kwa juhudi za kusaka amani ya kudumu nchini Somalia suala ambalo limekuwa likiendelea tangu kuangushwa kwa utawala wa Siad Barre miaka zaidi ya 20 iliyopita.

Wiki hii amelifahamisha baraza la usalama juhudi za jumuiya ya kimataifa na hususani Umoja wa Mataifa zimeanza kuzaa matunda Somalia, kwanza kundi la wanamgambo wa Kiislam la Al-Shabaab limefunga virago na kukimbia Moghadishu.

Pili Rais na spika wa Bunge waliokuwa na mfarakano kwa muda sasa wameshikana mkono na zaidi ya hapo wako tayari kumaliza kipindi cha serikali ya mpito na kufungua ukurasa mpya katika amani ya kudumu ya Somalia. Mkuu wa Idhaa hii Flora Nducha ameketi na balozi Mahiga  kujadili hatua hizo.

(MAHOJIANO NA BALOZI MAHIGA)