Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanachama wa UM waombwa kuchangisha kusaidia waathiriwa wa utumwa

Wanachama wa UM waombwa kuchangisha kusaidia waathiriwa wa utumwa

Kando na kuwahakikishia elimu watoto wafanyikazi wanaopatika wamefungiwa kwenye viwanda vya mikeka na kuwasaidia watumwa wa ngono, mfuko wa fedha wa Umoja wa mataifa unaowasiadia walio kwenye utumwa pia umesaidia miradi kweye zaidi ya nchi 90 kuwa ya minafaa.

Mkuu ya haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay na mjumbe maalum kwenye masuala ya utumwa Gulnara Shahinian wametoa wito kwa wanachama wa Umoja wa Mataiafa kuchangia mfuko huo wa UM ili kuhakikisha kuwa miradi hiyo imeendelea kuwafaidi waathiriwa.

Pillay amesema kuwa kupambana na utumwa kama huu kunahitaji kushughulikia vyanzo vyake kama vile umaskini na ubaguzi.