Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu wanaokimbia mapigano Kordofan Kusini waingia Sudan Kusini

Watu wanaokimbia mapigano Kordofan Kusini waingia Sudan Kusini

Zaidi ya watu 8000 wamekimbilia taifa jipya la Sudan Kusini wakitoroka mapigano kwenye jimbo la Kordofan kusini. Wengi wanaokimbia ni wakimbizi kutoka milima ya Nuba iliyo kati kati mwa Sudan walioanza kuingia Sudan Kusini mwezi Julai kufuatia mapigano makali pamoja na mashambulizi ya anga.

Tangu wiki iliyopita kumekuwa na ongezeko la wanaokimbia mapigano huku takriban watu 500 wakiwasili kila siku. Adrian Edwards ni msemaji kutoka UNHCR.

(SAUTI YA ADRIAN EDWARD)