Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la usalama la UM limewateua tena waendesha mashtaka wa mahakama za uhalifu za UM

Baraza la usalama la UM limewateua tena waendesha mashtaka wa mahakama za uhalifu za UM

Baraza la usalama limewateua tena waliokuwa waendesha mashitaka wa mahakama za kimataifa za uhalifu zinazosimamiwa na Umoja wa Mataifa. Waendesha mashitaka hao wamekuwa na jukumu la kuwafikisha kwenye mkono wa sheria washukiwa wa uhalifu uliotekelezwa wakati wa vita vya Balkans miaka ya 1990 na mauaji ya kimbari ya Rwanda ya mwaka 1994.

Katika maazimio mawili tofati baraza limemteua tena Serge Brammertz wa mahakama ya uhalifu ya Yugoslavia ya zamani ICTY na Hassan Bubacar Jallow wa mahakama inayohusika na  kesi za mauaji ya kimbari ya Rwanda ICTR kwa muhula wa miaka mingine mitatu hadi December 31 mwaka 2014. George Njogopa anaripoti.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)