Waliouawa mjini Abuja wakuumbukwa na UM

15 Septemba 2011

Umoja wa Mataifa umeandaa sherehe za makumbusho mjini Abuja nchini Nigeria kwa wafanyikazi wake waliouawa wakati makao yake yaliposhambuliwa na mshambuliaji wa kujitoa mhanga mnamo mwezi uliopita.

Kupitia kwa ujumbe uliowasilishwa kwa niaba yake na maratibu wa Umoja wa Mataifa nchini Nigeria Daouda Touré katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ametoa wito wa kutolewa kwa heshima kwa wale ambao wamejitolea kuhakikisha kuwa huduma za UM zinaendelea nchini humo. Wafanyikazi 11 wa Umoja wa Mataifa na watu wengine 12 waliuawa na wengine 116 wakajeruhiwa kwenye shambulizi hilo la agosti 26.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter