Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwanakampeni waNamibia ashindi tuzo ya UM

Mwanakampeni waNamibia ashindi tuzo ya UM

Mwanakampeni wa watu maskini nchini Namibia, Kundi lililobuni njia ya chini ya ardhi ya kupunguza msongamano nchini Malaysia na taasisi moja nchini Namibia inayohusika na bidhaa rahisi za ujenzi ni baadhi ya washindi 6 wa tuzo la Umoja wa Mataifa la mwaka huu linalowatuza wale wanaochangia kwenye maendeleo na makao kwa watu.

Tuzo hilo lijulikanalo kama Scroll of Honour lililotangazwa na shirika linalohusika na makaazi la Umoja wa Mataifa la UN-HABITAT lilipewa watu binafsi au taasisi kutoka nchini Namibia, Malaysia, Cuba , Australia, Urusi na Marekani.