Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mapigano Blue Nile nchini Sudan yamewaacha mamia bila misaada:UN

Mapigano Blue Nile nchini Sudan yamewaacha mamia bila misaada:UN

Mamia kwa maelfu ya watu wameendelea kukwama kufutia kuzuka kwa mapigano baina ya vikosi vya serikali ya Sudan na kundi la waasi katika eneo la nchi hiyo linalojulikana Blue Nile. Kutokana na mapigano hayo wengi wa raia wanasota na kushindwa kufikiwa na huduma muhimu za dharura jambo ambalo linaangusha ustawi wao.

Kulingana na ripoti zilizotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia misaada ya kiutu na dharura OCHA, marafuku iliyowekwa na serikali ya kutoingia kwenye eneo hilo imefanya shughuli zote za utoaji misaada kusimama. Hapo awali mapigano hayo yaliarifiwa kuzuka katika eneo la kusini mwa jimbo la Kordofan lakini hali hiyo sasa imesambaa hadi katika maeneo jirani ya Blue Nile.