Idadi ya watu duniani kufikia bilioni 7 Oktoba mwaka huu:UNFPA

14 Septemba 2011

 

Idadi ya watu duniani itafikia bilioni 7 hapo Oktoba 31 mwaka huu, kiwango ambacho kitatoa fursa na changamoto kubwa kwa watu wote duniani limesema shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu UNFPA. Kwa ushirikiano na serikali mbalimbali, mashirika, taasisi na watu binafsi NFPA ndiyo inayoongoza kampeni hii kwa uzinduzi wa mpango wa kimataifa jlikanao kama 7billioni Action chini ya kauli mbiu “watu bilioni saba wakihesabiana”

Kampeni hiyo ambayo inatangazwa pia katika mtandao inaelezea hadithi binafsi na hisia kuhusu kufikia idadi ya watu bilioni 7 kwa lengo la kuchagiza kuchukuliwa kwa hatua na kuleta mabadiliko. Na kampeni hiyo leo kwenye Umoja wa Mataifa inaambatana na mjadala maalumu ukimshirikika Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon, mkrugenzi mkuu wa UNFPA Babatunde Osotimehin, wawakilishi kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, sekta binafsi na jumuiya za kijamii.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter