Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP na wizara ya mambo ya kigeni nchini Tunisia kwenye miradi ya kuwafaidi wananchi

WFP na wizara ya mambo ya kigeni nchini Tunisia kwenye miradi ya kuwafaidi wananchi

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP pamoja na wizara ya mambo ya kigeni ya Tunisia wamekubaliana kuwepo kwa WFP nchini humo na kuanzisha miradi ya kulipwa baada ya kufanya kazi ili kuwasaidia watu maskini nchini humo.

Miradi hii itawafaidi takriban watu 240,000 na familia 48,000 hasa kupitia kwa miradi ya kulinda maji na udongo pamoja na miradi mingine ya kuwaletea pato.