Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mafuriko yaikumba Pakistan

Mafuriko yaikumba Pakistan

Shirika la Umoja wa Mataifa la utabiri wa hali ya hewa WMO linasema kuwa idara ya utabiri wa hali ya hewa nchini Pakistan ilitoa utabiri mara mbili jana Jumatatu tarehe 12. Utabiri wa mwisho kabisa unaonyesha kuwa kutakuwepo mvua kubwa katika eneo la kusini mashariki mwa Sindh na Rajasthan nchini India.

Pia utabiri huo unaonyesha kuwa huenda kukashuhudiwa mvua kubwa kwenye nyanda za nchini za mkoa wa Sindh kwa muda wa siku tatu zijazo. Wakati huo huo shirika la mpango wa chakula duniani WFP huenda likaanza usambazaji wa chakula. Awali serikali ya Pakistan ilikuwa imeomba msaada wa kimataifa. Kwa sasa vikosi vya wanajeshi vinaendelea kuwahamisha waliokwama kwenye mafuriko.

Mwishoni mwa wiki WFP ilituma tani 6 za chakula kusaidia karibu watu 400,000 hata kama uharibifu wa barabara unatatiza juhudi za kuwafikia waathiriwa. Christiane Berthiaume ni msemaji wa WFP.

(SAUTI YA CHRISTIANE BERTHIAUME))