Rais wa zamani wa baraza kuu akumbukwa
Baraza kuu la Umoja wa Mataifa Jumatatu ya leo limemkumbuka Rais wake wa zamani Harri Holkeri aliyefariki dunia Agosti 7 mwaka huu.
Wakati baraza hilo likihitimisha kikao chake cha mwisho cha 65 kabla ya kesho kuanza kikao kipya cha 66 lilikaa kimya kwa dadika moja kwa heshima ya Bwana Holkeri ambaye alikuwa raia wa kikao cha 55 cha baraza hilo mwaka 2000 hadi 2001.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amemuelezea Bwana Holkeri ambaye alikwa pia waziri mkuu wa Finland kama mtu aliyekuwa muwajibikaji na mtazamo wa mbali katika kutimiza malengo ya Umoja wa mataifa.